Bi.
Sophia Mkazi na Mwenyeji wa Kijiji cha Kasanga Wilayani Kisalawe Mkoani
Pwani akiwakaribisha wageni ambao ni Washiriki wa Shindano la mama
shujaa wa Chakula kijijini huko katika sherehe ya iliyofanyika Kijiji
cha Makumbusho Jijini Dar es salaam Jana. ambapo Programu mzima
itaoneshwa katika Runinga ya ITV kila Siku kuanzia Tarehe
2.08.2015-21.08.2015 kuanzia saa 12 Jioni.
Bw.
Godia Kaimu Mwenyekiti wa Kijiji cha Kasanga akiwakaribisha Washiriki
wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula Shindano Linaloendeshwa na Oxfam
Tanzania kupitia Kampeni ya Grow Kijijini kwake.
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Kisalawe Bw. Ellioth Phillemon
akiwakaribisha washiriki wa shindano la Mama Shujaa wa Chakula Wilayani
Kisalawe.
Kikundi
cha Burudani na sanaa cha Rumumba Theatre wakiendelea na Burudani
wakati wa sherehe hizo za ukaribisho kijiji cha Makumbusho
Eluka
Kibona, Meneja
Utetezi na Ushawishi wa Oxfam akielezea kwa ufupi juu ya Mchakato mzima
wa Shindano la Mama shujaa wa chakula ambalo linalenga kuwawezesha
wakina mama kutambulika katika kilimo na kueleza Matakwa yao juu ya
kilimo endelevu.
Bi.
Mwanaidi Hamza ambaye anatoka katika Programu ya Big Result now akitoa
ushuhuda jinsi gani alivyofanikiwa kulingana na Proramu hiyo na sasa
anamaisha mazuri, na kuwasihi wakina mama wasikate tamaa katika kilimo.
Mkurugenzi
Msaidizi Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Jackson
Samwel akiwapongeza Shirika la Oxfam kupitia kampeni yake ya Grow
kuanzisha shindano la Mama shujaa wa Chakula , kwa kutambua umuhimu wa
ardhi katika kuzalisha chakula, ameshauri akinamama wabadilishane uzoefu
pindi watakapokuwa kambini ili kuja na mbinu mpya za kilimo, ufugaji na
uvuvi.
Mmoja wa watoa Burudani, Mwanamke huyu akionesha kuhusu swala zima la Kilimo Endelevu.
Stephen
Mfuko aka Zero akitaja namba za washiriki na Jinsi ambavyo wanaweza
Pigiwa Kura ambapo Programu mzima itaoneshwa katika Runinga ya ITV
kila Siku kuanzia Tarehe 2.08.2015-21.08.2015 kuanzia saa 12 Jioni.
Wageni waalikwa katika sherehe hiyo
Ofisa
wa Programu ya Kampeni ya Grow Tanzania Suhaila Thawer akitoa maelezo
mafupi ya Mchakato rasmi wa kumsaka Mshindi wa Mama shujaa wa Chakula
Wanao
onekana Mbele ni Baadhi ya wenyeji ambao ndio watakuwa wenyeji wa
washiriki wa mama shujaa wa chakula pindi watakapokuwa kijijini.
Mkurugenzi
Mkazi wa Oxfam Tanzania Jane Foster akiwashukuru wadau mbalimbali ambao
wamefanikisha mchakato mzima wa kuendesha shindano la Mama Shujaa wa
Chakula, Pia Kipekee Amewashukuru wafanyakazi wa Oxfam akiwepo Eluka
Kibona na Suhaila Thawer kwa kuwa Mstari wa mbele kufanikisha Shindano
hili na Mwisho kuwatakia kila Laheri washiriki wote wanaokwenda katika
kushindana kumpata Mama Shujaa wa Chakula.
Washiriki
wa Shindano la Mama shujaa wakiwa wanatambulishwa Tayari kuelekea
Kisalawe Kijiji cha Kisanga kwa ajili ya kumsaka mshindi ambapo Programu
mzima itaoneshwa katika Runinga ya ITV kila Siku kuanzia Tarehe
2.08.2015-21.08.2015 kuanzia saa 12 Jioni.


0 comments :
Post a Comment