- Written by @nkupamah blog
Meneja
Mshauri wa Zantel, Charles Jutta akizungumza na waandishi wa habari
mara baada ya kukabidhi msaada wa vifaa vya usafi kwa mkoa wa Tanga,
kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mheshimiwa Magalula Said
Magalula.
Mkuu
wa Wilaya ya Tanga Abdula Lutavi akiteta jambo na Meneja Mshauri wa
Zantel, Charles Jutta
(Kushoto) mara baada ya makabidhiano ya vifaa vya
usafi baina ya Zantel na jiji la Tanga anayeshudia katikati ni meneja
mauzo wa Zantel Tanga.
Mkuu
wa mkoa wa Tanga Magalula Said Magalula (kulia) akishiriki zoezi la
usafi katika eneo la Mwembe Mawazo jijini Tanga muda mfupi baada ya
kupokea vifaa vya kufanyia usafi kutoka kampuni ya Zantel kushoto ni
Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mheshimiwa Abdula Lutavi.
Kampuni
ya simu za mkononi ya Zantel jana imetoa msaada wa vifaa vya usafi kwa
halmashauri ya jiji la Tanga venye lengo la kusaidia shughuli za usafi
katika jiji hilo.
Akizungumza
wakati wa makabidhiano hayo, Mkuu wa Mahusiano ya Serikali wa Zantel,
Bwana Charles Jutta alisema msaada huo ni sehemu ya juhudi za kampuni
yake kuziunga mkono jitihada zinazofanywa na halmashauri ya jiji la
Tanga katika kutunza na kuweka mazingira safi na salama kwa wakazi wake.
‘Kampuni
ya Zantel inaamini katika kushirikiana na serikali ili kuhakikisha
jamii yetu inaishi katika mazingira safi na salama, na vifaa hivi
tulivyotoa leo vitasaidia swala la usafi jijini hapa kama sehemu ya
wajibu wetu kwa jamii’ alisema Jutta.
Akiongelea
sababu za kampuni yake kushirikiana na manispaa ya jiji la Tanga, Jutta
alisema kuwa imani ya kampuni ya Zantel ni kuhakikisha mazingira
yanatunzwa ili kuhakikisha jamii inakuwa na afya bora na ustawi.
‘Mazingira
ndio hutoa taswira ya jamii husika, na sisi kama Zantel tunaamini jamii
isiyoishi kwenye usafi sio tu iko katika hatari ya kupata magonjwa,
bali pia haitaweza kustawi sawasawa’ alisema Jutta.
Akizungumza
wakati wa kupokea vifaa hivyo, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mheshimiwa
Magalula Saidi Magalula alisema msaada huo unaenda sambamba na jitihada
za ofisi yake katika kushughulikia kuboresha usafi wa mkoa wake.
‘Kwanza
niwashukuru Zantel kwa kutambua juhudi zetu na nitumie fursa hii
kuzitaka kampuni zingine kuiga mfano huu. La pili niwahakikishie kuwa
tumepata vifaa hivi wakati mwafaka kwani taarifa za mlipuko wa
kipindupindu zipo Dar es Salaam, zipo Morogoro na mikoa hii ina
mwingiliano mkubwa na sisi kwa hiyo vifaa hivi iwe changamoto kwa sisi
kuongeza kasi ya kufanya usafi zaidi, kila jumamosi wananchi tuendelee
kushiriki katika shughuli za kufanya usafi’ alisema Magalula
Mheshimiwa
Magalula ameishukuru kampeni ya Zantel kwa msaada huo huku akitaka
makampuni mengine nayo yajitokeze kuunga mkono juhudi za manispaa yake.
‘Jiji
letu limekuwa likikipa kipaumbele kikubwa swala la usafi, na leo
tunaishukuru kampuni ya Zantel kwa msaada huu, ambao tuna hakika
utasaidia katika kupeleka kasi swala la usafi hapa Tanga’ alisema
Mheshimiwa Magalula.
0 comments :
Post a Comment