- Written by @nkupamah blog
Mkimbizi akiaungusha kilio alipowasili katika kituo kikuu cha treni cha Dortmund, Ujerumani magharibi, Septemba 6, 2015.
Na RFI
Jumapili
mwishoni mwa juma hili, Ujerumani imekua ikikaribisha idadi kubwa ya
wahamiaji kutoka Hungary wakipitia Austria, kwa nyimbo, chakula na
mavazi. Hata hivyo, Vienna imetoa wito kwa Umoja wa Ulaya kutafuta
haraka jawabu la pamoja katika suala hilo.
Kutokana
na uzito wa mgogoro huo uliochochewa na migogoro katika Mashariki ya
Kati, Papa Francis amezitolea wito Jumapili Septemba parokia zote za
Kikatoliki barani Ulaya kila moja kupokea familia moja ya wakimbizi.
Polisi ya
Ujerumani imetoa idadi kubwa ya wakimbizi wapya 10,000 waliowasili
nchini humo wakitokea Austria kwa siku ya Jumapili mchana pekee, baada
ya kuorodhesha wakimbizi wengine 7,000 siku moja kabla, ambao wamekua
wakipokelewa kila mahali na majeshi ya kujitolea kwa mabango
yalioandikwa "Karibu Ujerumani".(P.T)
" Watu
wanatuhudumia vizuri hapa, wanatuhudumia kama binadamu, si kama nchini
Syria ", amesema Muhammad, mkimbizi mwenye umri wa miaka 32 kutoka mji
wa Syria wa al-Qusayr unaoendelea kukumbwa na machafuko.
Katika
mji wa Frankfurt, usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili, umati wa watu
wakiimba " Huu ni mshikamano wa kimataifa ", huku kukiwa na makofi na
kushangilia, wamekua wakiwapokea watu ikiwa ni pamoja na wanaume,
wanawake na watoto, ambao wameonekana wamechoka na safari yao ndefu.
Wakati
ambapo Ulaya ikigawanyika, kwa sasa inakabiliwa na migogoro mibaya zaidi
ya wahamiaji tangu mwisho wa Vita vikuu vya II vya dunia, Berlin kwa
upande wake imelegeza sheria zake kwa kuwapokea raia kutoka Syria, huku
ikipinga uamzi wa kuwarejesha katika eneo lao walikoingilia barani
Ulaya.
Katika
uamuzi usiyokuwa wa kawaida, Austria ilikubali usiku wa Ijumaa kuamkia
Jumamosi, kwa ushirikiano pamoja na Berlin, kuwarahisishia maelfu ya
wakimbizi waliozuiliwa nchni Hungary kwa mapokezi na sehemu za kupitia
ili kuingia Ujerumani Hungary ilishuhudia wimbi la wakimbizi 50,000
walioingia nchini humo kwa mwezi wa Agosti pekee.
Uamuzi
huu hata hivyo ni wa "muda", ameonya Jumapili, Kansela Werner Faymann,
akibainisha kuwa "uamzi wa aina hii haiwezi kuwa suluhu ".
Katika
mahojiano ya simu Jumamosi, Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na Waziri
mkuu wa Hungary, Viktor Orban, walikubaliana kwamba Hungary na
Ujerumani wanatakiwa kutimiza wajibu wa Umoja wa Ulaya " na kwamba wimbi
hili la wakimbizi lililoshuhudiwa mwishoni mwa wiki hii limekua la
kipekee", amesema Kansela Angela Merkel.
0 comments :
Post a Comment