Friday, October 23, 2015
@nkupamah blog
BARAZA
la Wanawake la Chama Cha Demokrasia (Chadema) Taifa, Bawacha,
limewataka wanawake nchi nzima kupiga kura na kukaa mita 200 ili kulinda
kura zao kwani ni haki yao kisheria.
Kauli
hiyo imetolewa juzi na Naibu Katibu Mkuu wa Bawacha Kunti Yusuph wakati
wa mkutano na wanawake, uliofanyika katika ofisi za Chadema kanda ya
ziwa Victoria jijini Mwanza.
Mkutano
huo uliohudhuliwa na wanawake wengi na kusababisha watu walio wengi
kukosa eneo la kukaa kutokana na kunyimwa Uwanja wa Baptist uliopo kona
ya Bwiru na halmashauri ya manispaa ya Ilemela, dakika za mwisho licha
ya kuwepo taarifa.
Kunti
alisema kwa mujibu ya sheria ya uchaguzi ya mwaka 2010, inamruhusu mtu
kupiga kura na kukaa mita 200, kutoka kwenye kituo lakini serikali ya
CCM inawakataza wananchi kwa kisingizio cha usalama kitendo ambacho ni
kinyume na sheria.
“Katika
Taifa lolote lile haijawahi kutokea kwamba ukipiga kura uende nyumbani,
ndiyo mara ya kwanza kuona kwa Tanzania, hatuwezi kuondoka tutabaki
mita 200,” alisema Yusuph.
Kunti
ambaye ni mratibu wa mikutano ya kukutana na wanawake ya mke wa Mgombea
Urais wa Chadema, Edward Lowassa, Regina Lowassa, alisema kuwa kupitia
wanawake wa Mwanza, wanawake nchi nzima wanapaswa kupiga kura na kulinda
kura zao.
Alisema
endapo wanawake na watanzania kwa ujumla watapiga kura na kuondoka
watakuwa wamevunja sheria ya nchi hivyo amewaomba kulinda kura zao kwani
ndio maisha yao.
Kwa
upande wake Mama Regina Lowassa, alikivaa Chama cha Mapinduzi (CCM)
kushindwa kuongea ni nini watawafanyia watanzania na badala yake
wamegeuka watukanaji jukwaani.
“Kama
CCM wana nia njema na watanzania, kwa nini wasimame jukwaani na kuanza
kutukana ninawaomba Wanawake msitishike na watu wa aina hiyo,” alisema Mama Regina.
Pia
alisema kuna watu wachache ambao wamekusudia kuharibu uchaguzi kwa
lengo la manufaa yao binafsi kitendo ambacho watanzania wanapaswa kuacha
kukata tamaa.
Hata
hivyo Regina aliwaomba wanawake na watanzania kwa ujumla kukichagua
Chadema kuanzia ngazi ya Udiwani, Ubunge na nafasi ya Urais kwa
maendeleo ya Taifa.
0 comments :
Post a Comment