Published @nkupamah blog
Juhudi za
Mbabazi na Besigye kutaka kuafikiana mmoja wao ashindane na Museveni
zimegonga mwamba Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema wagombea urais
wanaoshindana naye kwenye uchaguzi mkuu mwaka ujao si tishio kwake.
“Hiki hakitakuwa kinyang’anyiro kikali,” ameambia kikao cha wanahabari mjini Kampala.
Wapinzani wakuu wa Bw Museveni wanatarajiwa kuwa Amama Mbabazi na Kizza Besigye, ambao walikuwa marafiki wake wakuu wak
ati mmoja.
"Nasikia
watu wakizungumza kuhusu kupiga vita ufisadi. Utawezaje kukabiliana na
ufisadi ilhali twasikia ukiomba huyu na yule wajiunge nawe?” amesema.
"Lazima uwe na uwezo,” ameongeza Bw Museveni.
Hii ni mara ya kwanza kwa Bw Mbabazi, aliyekuwa waziri mkuu wakati mmoja, kuwania urais.
Bw Museveni ameongoza Uganda tangu 1986
Museveni
aliwasilisha karatasi za uteuzi kwa tume ya uchaguzi janaTume ya
uchaguzi ya Uganda imeidhinisha watu wanane kuwania urais mwaka ujao
wakiwemo Bw Museveni, Bw Besigye, Bw Mbabazi na Venansius Baryamureba.
Kampeni zitaanza Novemba. BBC
0 comments :
Post a Comment