Kiongozi wa muda mrefu nchini Gambia Yahya Jammeh, anasema kuwa ataondoka madarakani baada ya kukataa kukubali kushindwa.
Katika tangazo kwenye runinga, Jammeh alisema kuwa hakuna haja ya hata tone moja la damu kumwagika.Taangazo hilo linakuja saa kadha baada ya mazungumzo kati ya bwana Jammeh na wapatanishi wa Afrika Magharibi. Hata hivyo hakuna taarifa zaidi kuhusu yale yayoafikiwa.
Bwana Jammeh alishindwa kwenye uchaguzi wa mwezi Disemba na mrithi wake Adama Barrow tayari amesha apishwa.
Bwana Barrow amekuwa akiishi katika taifa jirani la Senegal kwa siku kadha.
Wanajeshi kutoka nchi za magharibi mwa Afrika ikiwemo Senegal wametumwa nchini Gambia wakitisha kumtimua bwana Jammeh madarakani.
Uamuzi wa bwana Jammeh kuondoka ulikuja kufuatia mazungumzo na marais wa Guinea na Mauritania.
0 comments :
Post a Comment