Aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa ameibukia katika Kanisa la KKKT wilayani Handeni mkoani Tanga, kushiriki ibada ya Krismasi na kutumia nafasi hiyo kushukuru wapiga kura katika Uchaguzi Mkuu uliopita.
Wakati
Lowassa akifanya hivyo, tayari Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametoa
agizo la kupiga marufuku mikutano ya walioshindwa uchaguzi, ikiwamo
kushukuru kwa kuwa haina tija.
Lowassa
alikuwa mgombea aliyeungwa mkono na muungano wa vyama vinne vya
Chadema, NCCR-Mageuzi, NLD na CUF, vilivyounda Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa).
Hata
hivyo, kauli hiyo ya Majaliwa ilipingwa na chama cha Chadema, ambacho
katika tamko lake kilisema inaonyesha namna CCM na Serikali yake
vinavyoshindwa kuelewa kwamba kuna uhusiano kati ya dhana ya demokrasia
ya vyama vingi na maendeleo.
Akiwa
katika kanisa hilo, Lowassa alipopewa nafasi ya kusalimia waumini,
alisema kuwa yeye ni muumini mwenzao na mara kwa mara amekuwa akienda
kusali hapo kila anapopata nafasi, hivyo aliomba ushirikiano wa karibu.
Lowassa
aliwashukuru wale waliompa kura kwenye uchaguzi uliopita kwa nafasi ya
urais na kuwataka kudumisha amani na upendo uliopo, kwani walikuwa na
imani naye ndiyo maana walimpigia kura.
Pia
aliomba kualikwa kwenye ufunguzi wa moja ya makanisa hayo ambayo
utafanyika siku chache zijazo, akisema yeye tayari ni mwenyeji wa
Handeni na atashiriki yale yote ambayo atashirikishwa.Lowassa aliwataka
Watanzania kutumia amani kama silaha ya kujiletea maendeleo yao na ya
taifa.
Lowassa
yuko mapumzikoni na familia yake katika shamba lake la mifugo lililopo
eneo la Mzeri huko Handeni, na aliwashukuru wakazi na wananchi kwa
kudumisha amani baada kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu.
Alisema wingi wa kura walizompa yeye na wagombea wa Ukawa ni kielelezo cha namna walivyokuwa na imani kubwa kwao.
Awali,
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la KKKT wilayani Handeni, Lewis Shemkala
aliwataka Watanzania kumrudia Mungu kwa kubadilisha maisha yao kwao
kufuata yale ambayo ameagiza kwa kuwa na roho ya imani na yenye huruma.
Shemkala
alisema endapo watu watafuata miongozo ya kidini kwa kukabidhi maisha
yao kwa Mungu, hata mambo ya uharifu yatapungua nchini na wananchi
wataishi kwa amani na utulivu kama zamani
Kwa
upande wake mkazi wa mtaa wa Seuta na muumini wa kanisa hilo, Ndimmyake
Mwakibinga, alisema wamefarijika kusali na kiongozi huyo mkubwa katika
ibada hiyo.
Katika
ibada hiyo wananchi wengi walionekana kumshangaa sana Lowassa badala ya
kufuatilia ibada hali iliyoonyesha kuwa alikuwa kivutio kikubwa kwa
waumini wa kanisa hilo.
0 comments :
Post a Comment