Nkupamah media
Na Rabi Hume, Modewjiblog
Mchezaji
wa zamani wa Arsenal, Thierry Henry na mwenzake wa Liverpool, Jamie
Carragher ambao kwa sasa ni wachambuzi wa soka katika kituo cha michezo,
Sky Sports wamemshangaa kocha wa Manchester United, Louis Van Gaal kwa
jinsi anavyomtumia mchezaji wake, Antony Martial.
Wakiwa
katika kipindi cha michezo katika kituo hicho wakati wakimzungumzia
Martial kwenye mchezo wa
wikiendi iliyopita ambapo Manchester United
ilipoteza mchezo huo mbele ya Norwich kwa kipigo cha goli 2 kwa 1 ambapo
Henry alionekana kuuliza swali ambalo lilikuwa kama linamlenga kocha
Van Gaal kwa kusema “Unafanya nini hapa? Kiukweli sijui anafanya nini
pale”.
“Alitakiwa
kuwa pale (eneo la penati), akiwa karibu na kipa, anafunga na
kushangilia. Ndiyo sawa? Ni kwasababu wana uwezo mdogo sana? Naona hilo,
“Wanahitaji
mchezaji ambaye anafunga magoli, wanahitaji mchezaji amabye anaweza
kukimbia haraka amekuja na na vitu hivyo, ingawa anatafuta mwenyewe
mpira na hagusi kutoka kwa wenzake,
“Nahisi nikiwa na mchezaji kama yeye, atakuwa namba 9 yangu na wengine wote watakuwa nyuma yake,” alisema Henry.
Kwa
upande wa Carragher alisema “Hayo ni mapendekezo ya Van Gaal, yeye
kucheza pembeni [Martial]. Tusifanye kuwa tumesahau kuwa yule ni
mshambuliaji wa kati ambaye ana uwezo wa kuchukua mpira na kukimbia nao
akiingia ndani ya eneo la penati”
“Unaangalia
mara ngapi anagusa mipira? Hagusi mpira kabisa ndani ya eneo la penati
na anapiga mpira mrefu mmoja tu, kwahiyo hana madhara akiwa pembeni na
kusababisha mashambulizi langoni kwake,
“Na haya
yote yanakuja kwa maelekezo kutoka kwa meneja, na ndiyo maana Manchester
United haionekani kuwa ikifunga magoli kwenye michezo yake”
Antony
Martial aliwasili Manchester United msimu huu akitokea Monaco ya
Ufaransa kwa kitita cha Pauni Milioni 36.7 ambaye alifanikiwa kufunga
magoli matano katika michezo yake tisa ya kwanza lakini kwa sasa hali
imekuwa ni tofauti kwa kufunga goli mbili katika michezo yake 11
iliyopita.(P.T)


0 comments :
Post a Comment