WANAJESHI WA IRAQ WAPIGA HATUA DHIDI YA IS

 Image caption Operesheni ya kuukomboa mji wa Ramadi ilianza Jumanne
Wanajeshi wa Iraq wamepiga hatua kwenye operesheni yao dhidi ya wapiganaji wa Islamic State mjini Ramadi.
Kasi yao imepunguzwa na mabomu yaliyotegwa katika mji huo, maafisa wa jeshi wanasema.
Wanajeshi hao ambao wanasaidiana na wapiganaji wa Kisuni wamo mita 500 kutoka afisi kuu ya baraza la mji.
Wamefanikiwa kukomboa mitaa kadha ya mji tangu kuanza kwa operesheni hiyo siku tano zilizopita.
Mji huo wenye Wasuni wengi umo kilomita 90 magharibi mwa Baghdad na ulitekwa na wapiganaji wa IS mwezi Mei.
Kutekwa kwa mji huo kuliaibisha sana jeshi la Iraq.
Wakati wa kuzinduliwa kwa operesheni Jumanne, jeshi la Iraq lilisema lilitarajia wapiganaji takriban 300 walio mjini humo wafurushwe katika kipindi cha siku kadha.
Lakini sasa kuna wasiwasi kwamba huenda wapiganaji hao wanashikilia mateka raia.
Wapiganaji wa IS wamepokonywa miji mingi waliyokuwa wameiteka nchini Iraq, huku wakiendelea kukabiliwa vikali na wanajeshi wa Iraq na wapiganaji wa Kikurdi.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment