ACT Wazalendo Watoa tamko na Onyo kali kuhusu Serikali kuzuia kuonyeshwa Matangazo ya Bunge.......Tusimruhusu Rais Magufuli Kusimika Utawala Wa Kidikteta Nchini- ACT Wazalendo

Nkupamah media:

JANA limetokea tukio la aibu katika nchi yetu pale serikali ilipofanya jaribio la hatari la kuzuia wananchi kuona na kusikia kinachoendelea bungeni.

Kitendo cha serikali ya CCM kuzuia kuonyeshwa moja kwa moja vipindi vya bunge katika televisheni ya taifa ni cha kijima na sisi chama cha ACT-Wazalendo tunakilaani kwa nguvu zetu zote.
 
Tunakitafsiri kitendo hiki cha serikali kama mwendelezo wa hatua na juhudi za Rais Magufuli za kuminya demokrasia na kusimika utawala wa kiimla.

Tunawasihi wananchi kusimama imara na kuzipinga jitihada zozote ovu za kuminya demokrasia nchini.
 
Tunawapongeza wabunge wazalendo wa upinzani kwa kusimama pamoja na kupinga nia ovu ya serikali ya kuua demokrasia katika nchi yetu.

Tunawatia shime wabunge wote wazalendo kuendelea kupigania maslahi mapana ya taifa letu.

ACT-Wazalendo! Taifa kwanza leo na kesho!

Imetolewa na;
Samson Mwigamba,
KATIBU MKUU.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment