Katibu Mkuu Wa Umoja wa Mataifa,,,,,,,,,,,,Ban Ki-moon ataka askari watumwe Burundi.....

  • Nkupamah Media:
Ban Ki-moon katika mkutano wa viongozi wa AUImage copyrightAFP
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amewaambia viongozi wa Afrika kwamba anaunga mkono pendekezo lao la kutuma askari 5,000 wa kuweka amani huko Burundi.
Alisema hayo katika mkutano wa viongozi wa nchi za AU nchini Ethiopia, ambako viongozi hao watapiga kura kuunga mkono au kukataa pendekezo hilo.
Rais wa Burundi , Pierre Nkurunziza, amelipinga pendekezo hilo - Burundi inasema
kutuma wanajeshi huko itaonekana kama uvamizi.
Uamuzi wa rais huyo kugombea muhula wa tatu wa uongozi ndiyo uliozusha ghasia za miezi kadha.
Kiongozi wa Gambia, Yahya Jammeh, ambaye alinyakua madaraka kwa kupindua serikali, alisema hatounga mkono pendekezo hilo iwapo Burundi haitoridhia.
Na rais wa Chad, Idris Deby, amepokea nafasi ya uenyekiti wa AU kutoka kwa kiongozi wa Zimbabwe, Robert Mugabe
CHANZO:BBC

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment