Bi Mkora Anaulizwa: " Kiberenge Kuwahi Au Kuchelewa, Tatizo Ni Nini?

Bi Mkora,
Tatizo ni nini kiberenge kinapowahi au kuchelewa kufika? Na kinapozimika njiani?

Isaak.
Mwananyamala.
JIBU:
Samahani sana kaka yangu uliyeuliza swali, naomba nikujibu swali lako uwanjani ili watu wengi wapate kunufaika, maana hilo tatizo unalolisema watu wengi wanalo na wanaona ni hali ya kawaida. Lakini hali hii ina madhara makubwa katika suala zima la mahusiano. Hebu fikiria ingekuwa ndio wewe kila linapofanyika hilo tendo ama mwenzio kishamaliza haraka au inamchukua muda wee mpaka unaona toba! hii karaha itaisha lini, ungelifanyaje?
Huo ndio mwanzo wa mtu kutafuta spea tairi/kucheat/ au kuwa na mahusiano ya pembeni. Sisemi kuwa wote wanaokumbwa na hali hiyo wenza wao wanatafuta faraja pembeni, hapana, msije mkatoana ngeu huko mkasema aah Bi Mkora kasema, na kwa vile yeye ni Kungwi basi ni kweli. Maana yake ni hivi ikiwa mtu anakuwa na kiu kila siku iko siku akikuta kisima cha maji baridi na matamu atakunywa!
Niko njiani kuzungumzia sababu mbali mbali zinazopelekea watu kuwa na mhusiano ya pembeni, nafikiri ni makala itakayokuja hivi karibuni na mojawapo ya hiyo sababu ni ... Soma zaidi kwa kubofya hapo chini..
kutoridhishana katika masuala. Lakini hebu tuliangalie hili kwanza, ni kwa nini hali hii inatokea? Mie naweza kusema kuwa sababu kubwa ni malezi na makuzi yetu, tumekuzwa katika kuliona tendo la ndoa ni kitu cha kufanya mara moja kisha ukaishia zako, ama unageuka upande wa pili unakoroma, bila kujali hisia za uliyenayo.
Pili tunaogopa kuonyesha hisia zetu za mapenzi kwa tunaowapenda kwa sababu tutaonekana wadhaifu mbele ya wale tuwapendao au ndugu na jamaa zetu, tunaogopa kuonekana "tumelishwa limbwata", kimsingi hali hii inakaa kwenye subconscious mind yetu yaani nyuma ya ubongo wetu kama nitakuwa nimetafsiri hilo neno vizuri kiasi mpaka linaathiri hali ya kuridhisana katika tendo la ndoa.
Tatu ni maisha kwa ujumla,, ugumu wa maisha na mambo mengi yanayotuzunguka yanatufanya tufanye hili tendo tumalize ili mradi limeisha nawe umetimiza wajibu. Hapa ndipo linakuja suala zima la mawazo, msongo wa mawazo (depression), mgandamizo wa akili (stress) na mambo kibao ambayo yanakuwa yanazunguka kichwani kwa mtu. Hali hii haijalishi uwezo wa mtu kina kila kundi lina pirika pirika zake katika maisha. Mtu anaweza kusema kuwa mimi sina hili tatizo lakini kwa maisha ya sasa sidhani kama inawezekana labda kama unafanya yoga na umeishakuwa mzoefu katika yoga na unaweza kushut down mambo mengine ukaconcentrate kwenye shughuli moja tu.
Sababu nyingine nayo ni ya msingi ni lishe, aina ya vyakula tunavyokula, na uzito wa miili yetu na ukosefu wa mazoezi, vinachangia sana katika hali hii. Kuna vyakula vingi hasa matunda, mbegu na mengineo vinasaidia katika kuboresha tendo la ndoa. Kama una uzito mkubwa nalo ni tatizo, na kama udhaifu pia nalo ni tatizo, lakini mazoezi ni kitu muhimu sana kwani yanajenga stamina, na kukupa uwezo wa kuhimili nguvu ya hilo zoezi, ukiwa sio mtu wa mazoezi hiyo marathon itakushinda. Hii ni mada pana sana na inazungumzia vyakula vingi ambazo vinasaidia kuamsha hisia ndani ya miili yetu kutokana na virutubisho vilivyomo, kwa mfano ndivi mbivu, ni nzuri sana kwa sababu zina pottasium, nazi, na vyingi vinginevyo, sio kungumanga na ngisi na pweza peke yake. Tutazungumzia hii mada kwa urefu na mapana siku nyingine. Lakini kwa kifupi utunzaji wa afya za miili yetu na kula vyakula vyenye kusaidia kuamsha hisia ni muhimu.
Mbali na mazoezi na vyakula ni suala zima la kuonyesha mapenzi kwa umpendae, labda hilo tendo useme kuwa unalifanya na watu ambao huna hisia nao, hapo kwa kweli siwezi kukusaidia, lakini kama uko na mkeo, ni wajibu wenu wote kuhakikisha kuwa safari haishii njiani kwa sababu kiberenge kimezimika ghafla. Na kwanini kiberenge kizimike ghafla wakati uko na Laaziz wako, ua la rohoni mwako, suuzo lako la roho, utulivu wako wote unatakiwa upatikane hapo na si kwingineko. Kama kuna mahala pengine unarushwa roho na kupewa utulivu kuna hatari ya kushindwa kupata utlivu nyumbani kwako.
Ndio eeh kuna wengine wanaogopa kufaidi tunda la mti wa kati kati majumbani mwao na kupata utulivu unaostahili wanawaona wake zao kama vile "wakwe" zao. Hapo kwako bwana umepewa ruhsa ya kujidai, na mwenzio naye amepewa ruksa ya kujidai tena kwa mfano mie Bi Mkora na Bwana Mkora wangu tuliita umati wa watu tukawaambia kuwa leo sisi ni mwili mmoja, sasa iweje mie leo nione aibu kuutumia mwili wangu? Na hili ndilo linalowakumba wengi utaona mtu anaona aibu hata kumshika mkono mkewe wakati wa kuvuka barabara, mwe! Sisemi eti muanze kushikana shikana barabarani au muanze kupigana mabusu barabarani hayo yako nje ya tamaduni zetu. Lakini ukiwa nyumbani kwako, hayo mambo ni muhimu kufanya ili kuweka ukaribu baina yenu. Usisubiri wakati ule mko kwenye uwanja wa Nakivubo kwa mechi, hapana, mshike bega, kiuno, mbusu hata akiwa jikoni anapika. Na yeye hali kadhalika akushike mashavu, bega hata ukiwa umekaa tu unaangalia TV. Chezeni hata michezo mbali mbali pamoja, hili ni mojawapo ya mafundisho ya dini yangu.
Mkifika wakati wa mechi ya Nakivubo huko nako si kufika na kuanza kucheza mechi, kupasha moto miili ni muhimu sana, na usione haya kumuuliza mchezaji mwenzio wa timu pinzani kama yuko tayari kwa mechi. Atakwambia na hata asiposema kwa mdomo hata kwa ushara tu utajua kuwa sasa mpira uwekwe kati kati ya uwanja tayari kwa mechi. Mechi ni dakika tisini au zaidi, usicheze chini ya dakika tisini kwani hakikisha mwenzio amefunga goli na ikiwezekana mfunge magoli wote pamoja. Hili linawezekana kutokana na kujizoeza na kuacha ubinafsi (self restraint)na kwa kuwa mnakuwa mmejiandaa. Hapo utakuta hakuna cha kiberenge kuwahi kufika wala kuchelewa kufika.
Kingine kuna suala zima la faragha na utulivu wa mahala inapochezwa mechi, namaanisha huo uwanja wenyewe wa Nakivubo, na ikibidi kama uwezo upo waweza badili viwanja kadri uwezavyo, kuna jikoni, sebuleni, bafuni, hata mwaweza toka nje ya hapo mkaenda hata shambani kwenu kama mna kibanda huko! Eeh mnashangaa nini kwani hao wanaokaa maeneo hayo hawachezi mechi? Si wanacheza tena wakibembelezwa na sauti za njiwa na chiriku na ndege mnana. Sio kila siku kuishi monotonous life, maisha yale yale, hayabadilik hata kidogo, ni hatari. Kwa mfano mara moja au mbili kwa mwaka, au hata zaidi kama uwezo unaruhusu kwa akiba mlojiwekea mnakwenda viwanja vya mbali kama National Stadium au hata CCM Kirumba huko Mwanza au hata kijijini kwenu ambako hakuhitaji gharama kubwa, japo wiki moja mnajidai huko. Tena hizo za kijijini mie ndio nazipenda sikawii kwenda kukata kuni na babu yenu Bw.Mkora porini, tutatafuta matunda pori huko, tukate kuni, na "kukata kuni" hasa!, tukirudi tushaoga mtoni tuko fresh!
Kwa ujumla ni suala zima la ubunifu na utundu basi kwenye mapenzi hakuna dawa wala uchawi!
Bi Mkora
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment