Ajali zilizosababishwa na kimbunga hicho
Kimbunga kikali cha
theluji kinachobashiriwa kuwa kikubwa zaidi kwa muda wa miaka mia moja
kimewasili katika
ufukwe wa Mashariki mwa Marekani.Eneo linalotarajiwa kukabiliwa vikali ni mji mkuu wa Washington DC, ambako hali ya hatari tayari imetangazwa.
Afisi za wafanya kazi wa Serikali na shule zilifungwa mapema na huduma za usafirishaji pia kusitishwa.
Mji wa New York pia umetangaza hali ya hatari ya hali ya hewa.
Kumekuwa na visa zaidi ya 1,000 vya magari kugongana katika Caroline Kaskazini pekee.
Eneo la washington DC likiwa limejaa barafu
Zaidi ya watu milioni 50 wameonywa kuwa watarajie barafu ya kina cha zaidi ya futi mbili, itakayoongezeka kutokana na kimbunga na upepo mkali utakaovuma saa chache zijazo.
0 comments :
Post a Comment