- Waziri mkuu wa Uhispania Mariana Rajoy
Waziri Mkuu wa muda wa Uhispania amekataa ombo la kuunda Serikali mpya.
Bwana
Rajoy, ambaye chama chake kisichopendelea mabadiliko cha Popular Party
kilishinda vitivingi vya Bunge, bila kuwa na idadi ya kutosha ya kuunda Serikali, katika uchaguzi wa mwezi uliopita, alikataa ombi la Mfalme Filipe kuwa aunde Serikali.
Kwa mara ya kwanza tangu demokrasia irejee nchini Uhispania, Mfalme alikuwa mwenyekiti wa mkutano ulioshirikisha vyama vya kisiasa vinavyopingana.
Waandishi wanasema kuwa huenda Mfalme huyo akamsihi kiongozi wa chama cha kisosholisti Pedro Sanchez kuunda serikali mpya.
0 comments :
Post a Comment