Serikali imesema leo kuwa mawaziri wakuu wastaafu waliokihama Chama cha Mapinduzi (CCM) na kuhamia vyama vya upinzani wataendelea kulipwa pensheni zao kwa mujibu wa sheria ya nchi bila kubaguliwa. |
Mawaziri wakuu hao; Fredrick Sumaye na Edward Lowassa walihama CCM na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Mandeleo (Chadema) na badaye Lowassa aligombea urais chini ya mwamvuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Akijibu maswali ya baadhi ya wabunge waliohoji endapo watu waliokuwa katika nyadhifa hizo wanaweza kuzuiwa kuchukua pensheni zao kwa kuhamia upinzani, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Utumishi wa Umma, Angellah Kairuki amesema sheria haizuii kwa kuwa kuhama chama ni haki ya kikatiba ya kila mtanzania.
Akinukuu Sheria ya mwaka 1999 pamoja na ile ya mwaka 2005 ya Utumishi wa Umma, Kairuki amesema waliokuwa viongozi katika nyadhifa hizo wana haki ya kuendelea kupata stahiki hizo kisheria.
Hata hivyo ameonya kuwa, wanapaswa kuheshimu sheria ya nchi inayowazuia kutoa siri za nchi wakati wakiwa katika nyadhifa zao.
About Unknown
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments :
Post a Comment