Amri iliyopiga
marufuku safari zote mjini New York wakati wa dhoruba kali ya theluji
katika mwambao wa Mashariki wa Marekani, imeondoshwa.
Madereva walikaidi amri juu ya hatari na kutozwa faini na hata wengine kukamatwa.Hata hivo, meya wa mji, Bill de Blasio, aliwasihi watu wajiepushe na safari zisokuwa za lazima, na wabaki ndani majumbani mwao.
Watu kama 18 wamekufa katika mmiminiko wa theluji na upepo mkali.
Malaki ya watu wamekosa umeme, na ndege chache tu zinatarajiwa kuondoka New York au Washington leo.
Maeneo makubwa ya mashariki mwa Marekani yamefukiwa na theluji .
Sasa usafiri wa reli na ndege uliokuwa umetatizwa umefunguliwa.
Zaidi ya watu 200,000 walibakia bila umeme.
Maeneo mengine yalishuhudia theluji yenye hadi urefu wa mita moja.


0 comments :
Post a Comment