Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angellah
Kairuki (Mb) (kushoto) akimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi
Prof. Joseph Semboje alipoitembelea taasisi
hiyo mapema leo.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angellah
Kairuki (Mb) (mstari wa mbele katikati) akiwa katika picha ya pamoja na
watumishi wa Taasisi ya Uongozi alipoitembelea taasisi hiyo mapema
leo.
……………………………………………………
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais –
Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki (Mb) ameielekeza Taasisi
ya Uongozi kufanya tathmini ya fursa za mafunzo zinazotolewa kwa
Watumishi wa Umma kama zinakidhi mahitaji ya nchi.
Waziri Kairuki alisema hayo leo alipokutana na Watumishi wa taasisi hiyo jijini Dar es salaam.
“Mafunzo yanayohudhuriwa na Watumishi wa Umm kwa mahitaji yetu”elekezaWazirinakuongeza niKairukijambolamsingi alikuainisha
maeneo yanayohitaji kuboreshwa katika eneo la kujenga uwezo ili kufikia malengo.
Waziri Kairuki alisisitiza kuwa
tafiti katika maeneo ya utoaji huduma kwa upande wa sekta ya umma zipewe
msukumo na mapungufu yatakayobainika baada ya tafiti kukamilika
yaelezwe bayana ili kupata kupata mrejesho.
Kwa upande wa viongozi wa umma
Mhe. Kairuki alisema ni vema wapate mafunzo katika masuala mtambuka ili
wafanye kazi kwa taratibu zilizowekwa.
Taasisi ya Uongozi, pamoja na
masuala mengine huendesha Programu za mafunzo kutokana na mapungufu
yanayoonekena kupitia tafiti mbalimbali zinazofanyika.
Taasisi ya Uongozi ilianzishwa kwa
ushirikiano baina ya Serikali za Tanzania na Finland na kutangazwa
katika gazeti la serikali la Tarehe 30 Juni, 2010.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Kny:KATIBU MKUU (UTUMISHI)
Kny:KATIBU MKUU (UTUMISHI)


0 comments :
Post a Comment