Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Wiliam Lukuvi kwa
niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe
Magufuli, akihutubia kwenye Mkesha Mkubwa Kitaifa,Dua Maalum ya
kuwaombea viongozi na Taifa uliofanyika kwenye uwanja wa Uhuru jijini
Dar es salaam.
Mchungaji
Eden Godfrey akihubiri kwenye Mkesha Mkubwa Kitaifa, Dua maalum
uliofanyika kwenye uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.
.
Umati wa wakazi wa jiji la Dar es salaam waliojitokeza kwenye ibada
maalum ya mkesha wa mwaka mpya uliofanyika kwenye uwanja wa Uhuru.
Wananchi wakiwa kwenye maombi ya kuliombea Taifa Amani, na kuwaombea viongozi wake afya njema.
Mwalimu Teddy Kwilasa akitoa maombi maalum kwa Taifa kwenye mkesha wa mwaka mpya.
Wananchi wakiwa kwenye maombi mazito ya kuwaombea Viongozi wa Taifa letu
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi (wa pili
kulia) akiwa pamoja na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Mhe. Nape Nnauye pamoja na wake zao wakiupokea mwaka kwenye Mkesha
Mkubwa Kitaifa, ambapo Taifa na Viongozi wake waliombewa.
Sehemu ya Vijana waliojitokeza kwenye mkesha mkubwa uliofanyika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akitoa salaam
maalum za kuwataka wazazi kuwafundisha watoto wao umuhimu wa amani ya
nchi wakati wa mkesha wa mkubwa kitaifa wa kuombea Taifa na Viongozi
wake dua maalum.
Bi. Christina Elias wa Aleluyah kwaya kutoka Tabata akiimba kwa hisia
kwenye mkesha mkubwa wa kitaifa kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es
Salaam.
Viongozi wakiwa kwenye maombi maalum ambapo waliwakilisha Mawaziri wote nchini.
0 comments :
Post a Comment