Tume ya Taifa ya haki za Binadamu Nchini Kenya imesema, jumla ya watu 37 walipoteza maisha baada ya kuzuka kwa machafuko ya baada ya Uchaguzi Mkuu nchini humo mwezi Agosti mwaka huu.
Tume hiyo imesema takwimu hizo zimekusanywa kipindi chote wakati machafuko hayo yakitokea kati ya tarehe 9 na 15 mwezi Agosti katika ngome za upinzani Magharibi mwa nchi hiyo na jijini Nairobi.
Imebainika kuwa, watu waliopoteza maisha walikabiliana na polisi wa kupambana na ghasia na kusababisha watu wengine 126 kujeruhiwa.
Maeneo yaliyoathiriwa wakati wa machafuko hayo ni mitaa iliyo na wafuasi wa upinzani jijini Nairobi ikiwemo Kawangware, Mathare, Kibera, Lucky Summer, Baba Dogo na Huruma.
Mtoto wa miezi sita Samantha Pendo, ni miongoni mwa watu waliopoteza maisha katika vurugu zilizozuka baada ya Tume ya Uchaguzi kumtangaza Uhuru Kenyatta kama mshindi wa Uchaguzi wa urais nchini humo.
Ripoti hiyo ya zaidi ya kurasa 600, imeeleza kuwa watu walipoteza maisha walikuwa na umri wa kati ya miaka 20 na 45
0 comments :
Post a Comment