Maafisa wa afya
nchini Uingereza wanatarajiwa kutoa mwongozo mpya kuhusu unywaji pombe,
ambapo watapendekeza watu kutokunywa pombe angalau siku mbili kwa wiki.
Mwongozo huo utatolewa baada yakutathminiwa upya kwa mwongozo wa awali uliotolewa miaka 20 iliyopita.
Ripoti zinasema afisa mkuu wa matibabu Uingereza Sally Davies atapendekeza watu wawe wakijizuia kunywa pombe angalau siku mbili kwa wiki.
Kiwango salama cha wanaume kunywa kwa siku pia kitapunguzwa na kufikia kilichopendekezewa wanawake.
Kwa sasa, wanawake hushauriwa kutokunywa zaidi ya vipimo 2-3 (sawa na gilasi ya mililita 175 ya mvinyo) kwa siku na wanaume vipimo 3-4.
Kipimo kimoja cha kileo ni sawa na nusu painti ya pombe isiyo kali sana au lager ya 4.5%, au mililita 25 za pombe kali.
Gilasi moja ya mililita 175 ya divai ya ukali wa 12% ina vipimo 2.1 na painti ya bia kali (ABV 5.2%) ina vipimo vitatu.
Mwongozo nchini Scotland tayari hushauri watu kujizuia kunywa pombe angalau siku mbili kwa wiki.
Mwongozo huo wa unywaji pombe ulianzishwa 2013 baada ya Idara ya Afya Uingereza kusema ilikuwa imepokea “malalamiko” kutoka kwa wataalamu wakipendekeza uchunguzi wa kina kuhusu pombe na afya.
0 comments :
Post a Comment