Mchezaji Bora wa Afrika wa wachezaji wanaocheza ligi za ndani na nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta ametuma picha katika ukurasa wake wa Twitter akiwasili mji mkuu wa Ubelgiji, Brussels kwa ajili ya kukamilisha dili lake la kujiunga na klabu ya Genk.
Safari ya Samatta nchini humo imekuja baada ya klabu yake ya TP Mazembe kuridhia mchezaji huyo kujiunga na Genk ambapo awali ilionekana kutokuwa tayari kumuachia nyota
huyo wa wachezaji wa ligi za ndani Afrika ambaye mkataba wake na TP Mazembe ulikuwa ukimalizika mwezi Aprili.
Samatta 2