![]() |
Wizara ya mambo ya nje nchini Tanzania imekanusha taarifa kwamba Rais John Magufuli amepiga marufuku uvaaji wa sketi fupi maarufu kama vimini. |
Taarifa ya Wizara hiyo imesema: "Ni
kweli kwamba Rais Magufuli na Serikali yake wanaunga mkono uvaaji wa nguo za
staha, lakini taarifa kwamba Rais Magufuli amepiga marufuku uvaaji wa sketi
hizo fupi si za kweli.”
Tangu Jumatatu wiki hii, mitandao ya
kijamii ilirindima na taarifa kwamba Rais Magufuli ametangaza marufuku hiyo.
Wizara ya Mambo ya Nje imelishutumu
gazeti moja la Kenya kwa kuanzisha uvumi huo, na kukiita kitendo hicho kuwa
"si cha umakini”.
"Wakati serikali ikifurahishwa na
taarifa nzuri za utaendaji kazi wa Rais Magufuli katika vyombo vya habari vya
Kenya na ulimwenguni kote, Wizara ya Mambo ya Nje imekerwa na utoaji wa taarifa
potofu na zisizo makini kama hii ihusuyo sketi fupi," imesema sehemu ya
taarifa hiyo.
Wizara hiyo hata hivyo imesema inaamini
habari hizo hazikuchapishwa gazetini makusudi.
About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments :
Post a Comment