- Haiti
Tume ya uchaguzi
nchini Haiti imearisha marudio ya uchaguzi wa urais kwa miaka mitatu
sasa, licha
ya Rais Michel Martly kutangaza kuwa uchaguzi huo
utaendelea.Tume ya uchaguzi ilisema kuwa ilifanya uamuzi huo kutokana na ukosefu wa usalama.
Kumekuwa na hali ya wasiwasi juu ya marudio ya uchaguzi huo wa Urais, kukiwa na maandamano ambapo makundi ya upinzani yamedai kuwa kuna njama ya kuiba kura.
Utawala wake unamalizika kikatiba baada ya majuma matatu na kuna hofu kuwa uchaguzi usipofanywa huenda kukazuka ghasia.
0 comments :
Post a Comment