Vita vyaathiri elimu ya watoto Sudan Kusini



Watoto Sudan kusini
Shirika linaloshughulikia watoto la Umoja wa Mataifa limesema zaidi ya nusu ya watoto Sudan kusini hawako
shule.
Kwa mujibu wa UNICEF, idadi hiyo ni kubwa kuliko nchi yoyote ile duniani.
Shirika hilo limesema watoto wa kike na wakiume wapatao milioni 1.8 hawajapata elimu darasani.
Shirika hilo limesema toka kuzuka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2013 zaidi ya shule mia nane zimeteketea.
Serikali mjini Juba ilisaini mkataba na waasi mwezi Juni, lakini hata hivyo ghasia katika maeneo mengine ya nchi bado hazijakoma.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment