Waziri Mkuu Asisitiza Bungeni Leo Kuwa TBC Hawatarusha Live Matangazo ya Bunge..........Asema TBC Wenyewe waliomba kwakuwa hawana Uwezo wakujiendesha Serikali Imeridhia tu.

Nkupamah media

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kwamba matangazo ya bunge hayatarushwa yote live kama serikali ilivyosema jana na tayari hatua hiyo imekwisha kuanza.

Majaliwa ameyasema hayo alipokuwa akijibu swali la papo kwa papo la Mbunge wa Hai ambaye pia ni msemaji wa kambi ya upinzani Bungeni Freeman Mbowe aliyetaka kujua kwanini serikali imefanya maamuzi ya kuzuia wananchi wasione matangazo ya Bunge moja kwa moja.

Akijibu swali hilo Waziri Mkuu amesema kwamba uamuzi wa kutoonyeshwa kwa matangazo ya moja kwa moja uliombwa na chombo cha umma chenyewe kwamba hakina uwezo kujiendesha na uamuzi wao huo umeungwa mkono na serikali.

''Maamuzi ya chombo hiki yameungwa mkono na serikali na waziri Nape Nnauye amefanya kipindi maalum kuhusiana na jambo hilo na wananchi wameelewa vizuri na wameiunga mkono serikali kwamba matangazo yatarekodiwa na yatarushwa kama kipindi maalum usiku'' Amesema Waziri Majaliwa.

Aidha chombo cha umma kitakuwa kinarusha matangazo ya moja kwa moja kwa muda wa maswali na majibu kwa serikali na baada ya hapo matangazo yatarekodiwa na kurushwa katika kipindi kiitwacho leo katika Bunge.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment