Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amefuta mfumo wa uwekaji wa matokeo wa Grade Point Average (GPA) ulioanza kutumiwa na Baraza la Taifa la Mtihani( NECTA) mwaka 2014.
Mfumo
huo uliofuta ule uliokuwepo wa Divisheni na kuanza kutumika kwa kidato
cha Nne na Sita,uliletwa kwa kile kinachoelezwa kujaribu kupandisha
ufaulu baada ya kuonekana wanafunzi wengi wamefeli mtihani wa kidato cha
nne, hasa mwaka 2013.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana mjini Dodoma,Waziri Pfrof. Ndalichako
ambaye aliwahi kuwa Katibu Mtendaji wa NECTA,alisema Baraza hilo
limeshindwa kueleza sababu za kutumia mfumo huo, badala yake limeishia
kutoa utaratibu uliotumika tu.
"Kwa
mamlaka niliyo nayo chini ya kifungu cha 20 cha sheria ya Baraza la
Mitihani Tanzania, sura ya 107, naliagiza Baraza kufanya mapitio ya
mfumo unaotumika sasa wa wastani wa alama (GPA) kwa lengo la kurudi kwenye mfumo wa awali wa Divisheni.
"Aidha, viwango vya ufaulu vizingatie azma ya nchi ya kuelekea kwenye uchumi wa kati na Tanzania ya Viwanda" Alisema Profesa Ndalichako
Kuhusu
mtihani wa pili(paper two), ameitaka NECTA kuufuta kwa watahiniwa wa
kujitegemea ambao umeanzishwa kama alama ya maendeleo wakati ni mtihani
wa mwisho.
"Wizara
haiwezi kufikia azma ya kusimamia ubora wa elimu katika ngazi zote bila
kuhakikisha viwango vya ufaulu vinawezesha kutoa wataalam wenye stadi
na maarifa badala ya kuwa na wahitimu wengi wenye vyeti, lakini
hawakidhi mahitaji ya soko la ajira," alisema Profesa Ndalichako
Januari
7 mwaka huu, Waziri Ndalichako alitembelea NECTA na kuwataka watoe
ufafanuzi wa kuacha kutumia mfumo wa Divisheni na kutumia GPA. Pia
aliwataka watoe maelezo ya kuanzishwa kwa mtihani wa pili kwa watahiniwa
wa kujitegemea.
Hata hivyo alieleza kuwa maelezo waliyoyatoa NECTA yalijikita katika kueleza utaratibu badala ya sababu za kuutumia mfumo huo.


0 comments :
Post a Comment