ALI KIBA Afunguka Kuhusu Mapenzi yake na Jokate...Adai Watu Wanafikiria Tofauti

Nkupamah media:

Alikiba na Jokate Mwegelo wamekuwa wakihusishwa kuwa wapenzi kwa miezi kadhaa sasa lakini hawajawahi kukiri hadharani.


Uhusiano wao umekuwa ukionesha kuwa upo kwa picha zao tu wanazopost kwenye mitandao ya kijamii, lakini tofauti na couples zingine wamekuwa wakiupeuka sana kuweka sentensi moja kuwa ‘sisi ni wapenzi.’

Tumezungumza na Alikiba kutaka kuujua ukweli na huenda akawa ametoa ‘hints’ ya kukusaidia kuthibitisha kama kweli uhusiano wao upo. “Watu wanafikiria tofauti, mimi na Jojo ni close friends,” amesema Alikiba.

“Tunapendana, tunashauriana, tunashare vitu vingi in a good way and she is a nice girl, she is beautiful na anastahili kuwa hata na mimi, kwanini sasa unashangaa? Lakini kama nikiamua kufanya vitu kama hivyo naweza kukuambia ‘Jojo si my girlfriend’ sishindwi lakini sasa watu wako tofauti,” ameongeza.

“Mimi siwezi kuweka personal life yangu hadharani, watu watanijua mimi kama mwanamuziki Alikiba na kuwapa vitu ambavyo wanastahili kupewa.”
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment