Dr. Slaa Ajibu Mapigo....Akanusha Nyumba Yake Kupigwa Mnada Kisa Mkopo Aliochukua Mkewe Na Kumpa Mwanaume Mwingine

Nkupamah Media:


Katibu Mkuu wa Zamani wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbroad Slaa ametoa majibu kuhusu taarifa zinazoandikwa kwenye baadhi ya magazeti nchini pamoja na mitandao kuwa nyumba yake iliyoko Mbezi jijini Dar es Salaam inauzwa baada ya kushindwa kulipa mkopo wa Benki ikidaiwa kuwa mkewe aliuchukua na kumpa mwanaume mwingine.

Taarifa hizo zilieleza kuwa Mke wa Dk. Slaa, Josephine alichukua mkopo wa shilingi milioni 300 katika moja kati mabenki nchini na kushindwa kuirudisha fedha hiyo.

Dk. Slaa ambaye yuko nchini Canada akijiendeleza kimasomo, amekanusha taarifa hizo na kueleleza kuwa yeye na mkewe Josephine hawajawahi kuchukua mkopo katika benki yoyote nchini.

“Nataka nikuambie na uwajulishe Watanzania kwamba wala si mimi Dk. Slaa wala mke wangu, Josephine kwa wakati wowote ule hatujawahi kuchukua mkopo benki,” Dk. Slaa aliliambia gazeti la Mtanzania kwa njia ya simu.

“Tangu nitoke Bungeni sijawahi kuchukua hata senti moja benki, achilia mbali propaganda ya shilingi milioni 300.

" Hivyo, ni vizuri waliokupa taarifa wakupe undani ni benki ipi nilikopa au Josephine alikopa na ni shilingi ngapi na kwa nyaraka zipi. 

"Na ni vema ukafuatilia benki husika pia kama walikuwambia ni benki gani,” Mwanasiasa huyo mkongwe alieleza.

Dk. Slaa ambaye alitangaza mwaka jana kustaafu siasa, alisema kuwa anapanga kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wote walioandika habari hizo
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment