Kamari yamtoa Roho Mtanzania uko Nairobi, Kenya


Kijana mwenye umri wa miaka 28 mwenyeji wa wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro ameuawa katika jiji la Nairobi Kenya baada ya kuwaua watu wawili kwenye Casino.

Watu walioshuhudia tukio hilo wamesema kijana huyo alikuwa amepoteza dola 300 za kimarekani baada ya kucheza kamari.

Baada ya hapo alijaribu kumsihi mwenye Casino arudishe pesa yake kwa kuweka simu yake rehani ndipo akaambiwa simu haikuwa na uwezo wa fedha hiyo ndipo akamchoma kisu mmiliki huyo na mlinzi wake katika mtaa wa Eastleigh.

Aidha baada ya kufanya tukio hilo umati wa watu ulimshambulia kwa kipigo na kusababisha kifo chake.

Jeshi la polisi limethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo kijana huyo alikuwa dereva bodaboda na inasemekana aliuza pikipiki yake na kucheza kamari katika Casino hiyo.
Chanzo BBC
You might also like:
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment