KATIBU MKUU MAMBO YA NDANI YA NCHI AFUNGUA WARSHA YA KUHAMASISHA SHERIA MPYA YA UDHIBITI UZAGAAJI WA SILAHA NA RISASI NCHINI

Nkupamah media:

ge1
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akizungumza na wajumbe (hawapo pichani) wa Warsha ya Kuhamasisha Sheria Mpya ya Udhibiti wa Silaha na Risasi katika Ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam. Wapili kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Wizara hiyo, Marlin Komba. Kulia ni Mwakilishi wa Katibu Mtendaji wa  Baraza la Mawaziri wa Nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika katika Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA), Esaka Mugasa. Katika hotuba yake, Katibu Mkuu aliwataka watu wanaomiliki silaha nchini isivyo halali kuzisalimisha haraka iwezekanavyo kabla ya operesheni ya kuwakamata haijaanza. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

ge2
Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Marlin Komba akizungumza na wajumbe (hawapo pichani) wa Warsha ya Kuhamasisha Sheria Mpya ya Udhibiti wa Silaha na Risasi katika Ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam, kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu ili aweze kuifungua warsha hiyo ya siku mbili. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
ge3
Mwakilishi wa Katibu Mtendaji wa  Baraza la Mawaziri wa Nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika katika Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA), Esaka Mugasa akizungumza na wajumbe (hawapo pichani) wa Warsha ya Kuhamasisha Sheria Mpya ya Udhibiti wa Silaha na Risasi katika Ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam. Watatu kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira na wapili kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Wizara hiyo, Marlin Komba. Katibu Mkuu katika hotuba yake ya ufunguzi wa warsha hiyo, aliwataka watu wanaomiliki silaha nchini isivyo halali kuzisalimisha haraka iwezekanavyo kabla ya operesheni ya kuwakamata haijaanza. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
ge4
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (wapili kulia) akitoka katika Ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam mara baada ya kufungua Warsha ya Kuhamasisha Sheria Mpya ya Udhibiti wa Silaha na Risasi. Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Wizara hiyo, Marlin Komba, wapili kushoto ni Naibu Kamishna wa Jeshi la Polisi-Makao Makuu, Hezron Gyimbi na kulia ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Yusuph Ilembo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
ge5
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akizungumza na wajumbe wa Warsha ya Kuhamasisha Sheria Mpya ya Udhibiti wa Silaha na Risasi katika Ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam. Katika hotuba yake, Katibu Mkuu aliwataka watu wanaomiliki silaha nchini isivyo halali kuzisalimisha haraka iwezekanavyo kabla ya operesheni ya kuwakamata haijaanza. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
ge6
Sehemu ya wajumbe wa Warsha ya Kuhamasisha Sheria Mpya ya Udhibiti wa Silaha na Risasi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (hayupo pichani) wakati alipokuwa akizungumza na wajumbe hao katika Ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam kabla ya kuwafungulia warsha yao ya siku mbili itakayojadili umasishaji wa Sheria Mpya ya Udhibiti wa Silaha ya Mwaka 2015. Hata hivyo, katika hotuba yake, Katibu Mkuu aliwataka watu wanaomiliki silaha nchini isivyo halali kuzisalimisha haraka iwezekanavyo kabla ya operesheni ya kuwakamata haijaanza. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
ge7
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (katikati waliokaa), Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Wizara hiyo, Marlin Komba (wapili kushoto waliokaa), Naibu Kamishna wa Jeshi la Polisi-Makao Makuu, Hezron Gyimbi (wapili kulia), Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Yusuph Ilembo (kulia) na kushoto ni Mwakilishi wa Katibu Mtendaji wa  Baraza la Mawaziri wa Nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika katika Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA), Esaka Mugasa, wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Warsha ya Kuhamasisha Sheria Mpya ya Udhibiti wa Silaha na Risasi. Warsha hiyo ya siku mbili ilifunguliwa na Katibu Mkuu, Rwegasira katika Ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment