Mabondia Francis Miyeyusho kushoto na Nassibu Ramadhani wakitambulisha mpambano wao utakaopigwa siku ya sikukuu ya pasaka katika uwanja wa ndani wa taifa katikati ni kiongozi wa ngumi Antony Rutta Picha na SUPER D BOXING NEWS
Kiongozi wa mchezo wa masumbwi nchini Antony Rutta katikati akiwainua mikono juu kuwatambulisha mabondia Francis Miyeyusho kushoto na Nassibu Ramadhani mbele ya waandishi wa habari Dar es salaam juzi kwa ajili ya kutambulisha mpambano wao wa pasaka katiku uwanja wa ndani wa taifa Picha na SUPER D BOXING NEWS
Mabondia Francis Miyeyusho kushoto na Nassibu Ramadhani wakitunishiana misuli mbele ya waandishi wa habari katikati ni kiongozi Antony Ruta wa pili kushoto ni Dei Miyeyusho na mwingine ni kocha Christopher Mzazi wakati wa kutangaza mpambano wa mabondia hawo siku ya Pasaka Picha na SUPER D BOXING NEWS
Na Mwandishi Wetu
MABONDIA Francis Miyeyusho na Nassibu Ramadhani wamesaini mkataba wa makubaliano wa kuzipiga siku ya sikukuu ya Pasaka katika uwanja wa ndani wa taifa jijini Dar es salaam
Akizungumzia mpambano uho mratibu wa mabambano hayo Rajabu Mhamila ‘Super D’ amesema kuwa amewasainisha mabondia hao kwa kuwa viwango vyao vipo juu sana katika kipindi hiki na ndio mpambano mkali utakaokuwa wa kufungua mwaka 2016
Aliongeza kwa kusema mbali na mpambano huo siku hiyo pia kutakuwa na mapambano mengine ya kukata na shoka ambapo mabondia mbalimbali watazipiga siku hiyo.
Mohamed Matumla atavaana na Cosmas Cheka wakati mabondia Mada Maugo atavaana na Abdalla Pazi katika mpambano wa nani zaidi kati yao pia bondia Vicent Mbilinyi atavaana na Mwinyi Mzengela na Pius Kazaula wa Morogoro atamenyana na Seba Temba.
Super D amewataka wapenzi wa mchezo wa masumbwi kujitokeza kwa wingi ili kushudia mpambano huo ambao unatarajiwa kuwa na msisimko wa aina yake, vilevile mabondia hao wamepanga kuanza ngumi hizo mapema ili wapenzi wafurahie mchezo huo mapema na kurudi majumbani na kujumuika na familia zao katika sikukuu hiyo hivyo ameomba mashabiki kufika mapema ili ngumi nazo zianze kwa wakati muafaka na kumalizika mapema.(P.T)


0 comments :
Post a Comment