Februari 16 kunatarajiwa kuanza kuchezwa kwa michezo ya hatua ya 16 katika Ligi ya Mabingwa Ulaya na baadhi ya vilabu tayari vimeanza kufanya mabadiliko ya vikosi ambavyo watavitumia katika michezo ya mashindano hayo.
Manchester City imetangaza kikosi chake ambacho itakitumia katika ligi hiyo kubwa barani Ulaya kwa vilabu na katika majina ambayo imeyaorodhesha kunaonekana kuwa na jina la Kelechi Iheanacho ambaye kwa siku za karibuni anaonekana kuwa na msaada mkubwa katika klabu hiyo.
kelechi-iheanacho-cropped_1u558s2pa1tkx1bgnuk5x3ymrb
Kelechi Iheanacho
Hata hivyo baada ya kuingia kwa jina la Iheanacho kuingia katika majina ya wachezaji wa Manchester City watakaocheza ligi ya mabingwa, jina la Samir Nasri limetolewa katika orodha hiyo na hilo linatokana na majeraha aliyonayo mchezaji huyo raia wa Ufaransa.
manchester-city-winger-samir-nasri_3360110
Samir Nasri
Majina ya wachezaji waliorodheshwa ni Sergio Aguero, Wilfried Bony, Willy Caballero, Gael Clichy, Kevin De Bruyne, Fabian Delph, Martin Demichelis, Fernandinho, Fernando, Joe Hart, Aleksandar Kolarov, Vincent Kompany, Eliaquim Mangala, Jesus Navas, Nicolas Otamendi, Bacary Sagna, David Silva, Raheem Sterling, Yaya Toure, Pablo Zabaleta, Kelechi Iheanacho.
Manchester City inataraji kucheza mchezo wake wa kwanza wa hatua ya 16 dhidi ya Dynamo Kiev, mchezo unaotarajiwa kuchezwa Februari 24.