Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea Afunguka Mazito Kuhusu Suala la Uchaguzi Zanzibar..'Nchi yetu itafika Pabaya'

Nkupamah Media:



Kubenea ameyasema hayo alipokuwa akichangia hoja ya mpango wa maendeleo bungeni
kwenye kikao cha 7 bunge la 11, na kusema kuwa suala la Zanzibar lisipochukuliwa hatua makini, litaipeleka nchi pabaya.

“Uchaguzi wa Zanzibar utatuletea matatizo makubwa kitaifa tusipokuwa makini, hakuna namna yoyote katika bunge hili ya kutozungumzia suala la Zanzibar, iwapo matatizo ya Zanzibar yasipotatuliwa kwa makini, mpango huu hautatekelezeka”, alisema Saed Kubenea.
Pia Saed Kubenea amesema watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini na mashirika m
balimbali ya kijamii yanaliona suala hilo, lakini wao kama wabunge hakuna ambaye amethubutu kuliongelea.

“Tunakaa kaa tu humu ndani, wakati maaskofu wanasema Zanzibar kuna tatizo, mashekhe wanaliona tatizo, tukajifanya hakuna matatizo, nchi yetu itafika pabaya na mpango wa maendeleo hautatekelezeka”, alisema Saed Kubenea
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment