Meek Mill Ahukumiwa Kifungo Tena


Meek-Mill-Main-Pub-1-James-DimmockMeek Mill 
RAPA maarufu duniani anayetoka jimbo la Philadelphia nchini Marekani, Meek Mill ameamuliwa kutumikia tena kifungo cha miezi mitatu nje ya jera, baada ya kukiuka masharti ya kifungo chake cha awali ambacho hakutakiwa kutoka nje ya jimbo hilo wala kufanya shoo yeyote nje na Marekani jambo ambalo yeye alikiuka mwezi Desemba.
Hukumu hiyo imetolewa jana Februari 2, na Jaji Genece Brinkley aliyekuwa akiendesha kesi yake.
Taarifa kutoka jarida la TMZ, rapa huyo mwenye umri wa miaka 28, ameamuliwa na mahakama kutumikia kifungo hicho kwa siku zisizopungua 90, huku akitakiwa kutorapu, kufanya shoo ya aina yeyote, au kutoa wimbo mpya kwa kipindi chote cha kifungo chake hicho.
FOX 29 imeripoti kuwa, Meek amepewa muda wa miaka sita kama muda wa matazamio kutokana na tabia zake chafu, endapo hatabadilika mwenendo wake basi mahakama itamchukulia hatua nyingine za kisheria.
Meek amekuwa kwenye muda wa matazamio tangu mwaka 2009 kuhusiana na skendo zake za madawa ya kulevya na matumizi mabaya ya silaha.
Mwezi Desemba, jaji alisema kuwa, Meek  alikaidi masharti ya kifungo chake ambayo hakutakiwa kusafiri nje ya jimbo lake lakini yeye aliondoka na kwenda “kula bata” mpenzi wake, Nikk Minaj huko New York na miji mingine ya Marekani bila kufanya mawasiliano ofisa wa mahakama.
Ameonekana mara mbili akienda mahakani hapo akiwa ameongozana na Minaj.
Meek Mill alitumia siku ya Alhamisi kukaa na kuzungumza na wanafunzi wa shule ya wavulana ya Latin of Philadelphia Charter.
Share on Google Plus

About mtilah

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment