MKURUGENZI MKUU WA TUME YA USHINDANI AKABIDHI VIFAA VYA MUZIKI KWA JESHI LA MAGEREZA

1Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani, Dkt. Fredrick Ringo akitoa maelezo mafupi kwenye hafla ya makabidhiano ya vifaa vya muziki kwa Uongozi wa Jeshi la Magereza. Hafla hiyo ilifanyikia Bwalo Kuu la Maafisa Magereza, Ukonga Jijini Dar es salaam, Januari 29, 2016.

2
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani, Dkt. Fredrick Ringo akimkabidhi Kamishna Jenerali wa Magereza John Casmir Minja gitaa la muziki ikiwa ni moja wapo ya vifaa vya muziki vilivyokabidhiwa kwa Jeshi la Magereza.
3
Kamishna Jenerali wa Magereza akijaribisha kupiga gitaa la muziki baada ya kukabidhiwa vifaa vya muziki katika hafla ya makabidhiano ya vifaa hivyo kutoka kwa Mkurugenzi wa Tume ya Ushindani, Dkt. Fredrick Ringo(wa kwanza kulia).(P.T)
4
Kamishna Jenerali wa Magereza John Casmir Minja akitoa neno la shukrani kwa Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani, Dkt. Fredrick Ringo kwenye hafla ya makabidhiano ya vifaa vya muziki ambavyo vitatumika kukuza vipaji vya Wanamuziki wa Jeshi la Magereza.
5
Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani, Dkt. Fredrick Ringo(hayupo pichani).
6
Baadhi ya vifaa vya muziki venye vilivyokabidhiwa kwa Jeshi la Magereza kama vinavyoonekana katika picha. Vifaa hivyo vitatumika kukuza vipaji vya Wanamuziki wa Jeshi hilo(Picha na Kitengo cha Habari, Makao Makuu ya Jeshi la Magereza).
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment