WASHUKIWA 50 WA AL-SHAHAB WAKAMATWA SOMALIA

Washukiwa 50 wa al-Shahab wakamatwa Somalia

  • Kamanda wa jeshi la polisi wa mji wa Johar nchini Somalia ametangaza kuwa watu 50 wametiwa mbaroni wakishukiwa kuwa na uhusiano na kundi la al Shabab.Sayad Ndje ameashiria vitisho vya kundi la al Shabab na kueleza kuwa, watu 50 wametiwa mbaroni wakishukiwa kuwa na uhusiano na kundi hilo. Watu hao wamekamatwa katika operesheni ya pamoja iliyofanywa na vikosi vya usalama vya Somalia na wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika katika mji wa Johar kwenye mkoa wa Shabelle ya Kati, huko kusini mwa Somalia.
Kundi la al Shabab ambalo limepoteza maeneo mengi yaliyokuwa chini ya udhibiti wake, lingali linaendeleza mashambulizi yake nchini Somalia na katika nchi jirani ya Kenya.(VICTOR)
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment