Nilijinyima ,Nillikuwa Nashindia Mihogo Mikavu Na Pilipili ,Niliogopa Kula Chips Kuku Pesa Zisije Zikaisha .Soma Habari Hii Ujue Ni Nani Aliesema Maneno Haya.

nkupamah media:


Msanii wa filamu na mjasiriamali, Salma Jabu aka Nisha amesema mafanikio aliyopata yametokana na kujinyima ambapo amedai ilifikia hatua alikuwa akishinda kwa kula mihogo huku akiogopa kula chipsi pesa zisije zikaisha.

Muigizaji huyo ambaye mpaka sasa ana filamu nane ambazo amezitoa kupitia kampuni yake ‘Nisha’s Film Production’, alikiambia kipindi cha Uhondo cha EFM kuwa alipitia changamoto nyingi mpaka kupata mafanikio aliyonayo sasa.

“Mimi nilianza na shilingi 50,000 tu pesa yangu ya kwanza ya filamu kulipwa, niliiweka na sikutumia hata shilingi kumi,” alisema Nisha.

“Mimi nilikuwa hata chakula saa nyingine nasema siwezi kula chipsi na kuku, hii acha hata ninunue muhogo mmoja halafu nyingine niweke akiba, ubahili wangu umesaidia. Leo nina biashara, kampuni ya filamu ya mamilioni na nimeajiri watu,” alieleza.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment