RAIS WA LIBERIA YUKO NCHINI UGANDA KWA AJILI YA UCHAGUZI

Nkupamah media:Sunday, 14 February 2016 

Rais wa Liberia yuko nchini Uganda kwa ajili ya uchaguzi
Rais Ellien Johnson Sirleaf wa Liberia yuko nchini Uganda kufuatilia uchaguzi mkuu wa nchi
hiyo ya Afrika Mashariki unliopangwa kufanyika wiki ijayo Februari 18.
Yvette Chesson-Wureh, Mjumbe Maalumu wa Sirleaf amefichua kuwa rais huyo wa Liberia yuko nchini Uganda chini ya timu ya waangalizi ya Women Situation Room, ambayo haiegemei siasa za upande wowote.
Shirika hilo la wanawake lilibuniwa kufuatia azimio nambari 1325 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ili kuhakikisha kuwa wanawake wanatoa mchango na kujihusisha kikamilifu na juhudi za amani na usalama katika mataifa mbali mbali duniani. Sirleaf ambaye ni mwanamke wa kwanza kuchaguliwa kuwa rais katika nchi hiyo ya Kiafrika, anahesabiwa kuwa shakhsia nambari sabini wa kike wenye uwezo mkubwa duniani, kwa mujibu wa ripoti ya Forbes za mwaka 2014.(VICTOR)
Tayari timu ya waangalizi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC chini ya uongozi wa Rais mstaafu wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi imewasili nchini Uganda. Uchaguzi mkuu wa Uganda unatarajiwa kufanyika Februari 18 na kiti cha urais kimewavutia wagombea 8 akiwemo Rais wa sasa, Yoweri Museveni. Hata hivyo mchuano mkali kwenye kiti cha urais unatarajiwa kuwa kati ya Museveni, Daktari Kizza Besigye wa chama cha FDC pamoja na Waziri Mkuu wa zamani, Amama Mbabazi ambaye anawania nafasi hiyo kama mgombea binafsi.CHANZO:IRAN SWAHILI
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment