Spika Wa Bunge Job Ndugai Akubali Kuzifumua Kamati Za Bunge.....Zitto Kabwe Kurudishwa PAC, James Mbatia Kamati Ya Bajeti

Nkupamah Media:


Baada ya malalamiko ya wabunge wa upinzani juu ya wajumbe wa kamati za kudumu za Bunge, Spika wa Bunge, Job Ndugai, anatarajia kuzipangua kamati hizo.

Taarifa za uhakika toka Bungeni mjini Dodoma zinasema, licha ya kuwapo kwa baadhi ya wajumbe walioomba kuhamishwa kwenye kamati walizopangiwa awali, kumekuwapo na mazungumzo kati ya
Kambi ya Upinzani Bungeni na kiti ofisi ya Spika juu ya suala hilo.

Inaelezwa kati ya wajumbe watakaohamishwa kutoka kwenye kamati zao za awali ni Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe aliyekuwa kwenye Kamati ya Maendeleo ya Jamii na sasa atapelekwa  Hesabu za Serikali (PAC).

Naye Mbatia aliyekuwa mjumbe wa Kamati ya Miundombinu, sasa atapelekwa kwenye Kamati ya Bajeti aliyokuwa akitumikia kwenye Bunge la 10.

Spika wa Bunge, alipotafutwa ili kuzungumzia suala hilo kupatikana.

Juzi Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bunge, Tundu Lissu, alisema wanafikiria kumpeleka Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, kwenye kamati ya PAC ili awe mwenyekiti wao.

“Wasipokubali (kubadilisha wajumbe) hatutakubali ungozi tutaacha, mimi mwenyewe sheria ndogo siendi, huko ni kupoteza muda kwa sababu hakuna kamati ya ovyo vile, nitaenda sheria na katiba na kushiriki mijadala, kura tu ndiyo sintopiga, hoja yoyote ya kisheria ikiibuka bungeni nitaibuka na watashangaa,” alisema Lissu.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment