Nkupamah media
Jacob Zuma
Umoja wa
Afrika umetangaza kwamba utawapeleka waangalizi 100 wa haki za
kibinaadamu pamoja na waangalizi wengine 100 wa kijeshi nchini Burundi.
Umesema kuwa rais wa taifa hilo Pierre Nkurunziza ameunga mkono mpango huo.
Rais wa Afrika kusini Jacob Zuma aliongoza ujumbe wa viongozi watano wa Afrika katika ziara ya siku mbili wiki hii.
Walikutana
na bwana Nkurunziza na viongozi wawili wa upinzani ambao wamesalia
nchini humo hata baada ya ghasia zilizozuka mwezi Aprili baada ya
Nkurunziza kutangaza kuwa atawania muhula wa tatu.
Wamesema kuwa mpatanishi wa AU rais Museveni wa Uganda ataanzisha mazungumzo hivi karibuni.BBC
0 comments :
Post a Comment