Timu pekee inayoiwakilisha Tanzania katika Ligi ya Mabingwa Afrika kwa vilabu, Yanga imefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli moja kwa bila katika mchezo wake wa awali wa ligi hiyo kubwa barani Ulaya kwa upande wa vilabu.

Goli la Yanga katika mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Currepipe Mauritius lilifungwa na Donald Ngoma katika dakika ya 17 ya kipindi cha kwanaza na kuweza kudumu hadi kunamalizika kwa mchezo huo.
Baada ya ushindi huo Yanga inarudi nyumbani kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania dhidi ya Simba mchezo utakaochezwa wikiendi ijayo na mchezo wa marudiano na Cercle de Joachim unatarajiwa kufanyika katika kipindi cha wiki mbili zijazo