Rafael Shilatu ambae ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Nyamagana (Kulia) akizungumza katika hafla ya kumpongeza
msanii Rich4D.
Chama
cha Mapinduzi CCM kimekubali kumsafirisha kwa ndege Mwanamuziki
Chipukizi Richard Stanford maarufu kwa jina la Rich4D, alietembea kwa
miguu kutoka Jijini Mwanza hadi Jijini Dar es Salaam ili kumpongeza Rais
Dkt.John Pombe Magufuli kwa kuwajumuisha Wasanii katika Wizara ya
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Mwenyekiti
wa Chama hicho Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza Raphael Shilatu,
alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita, katika hafla ya
kumpongeza msanii huyo kwa matembezi yake baada ya kurejea Jijini
Mwanza.
“Kwanza
nimpongeze kwa matembezi yake ambayo ni ya kizalendo kabisa. Lakini
niseme kwamba atakapopata fursa ya kwenda kuonana na Mhe.Rais,
tutamsafirisha kwa ndege kutoka Jijini Mwanza hadi Jijini Dar na
kumrudisha pia”. Alisema Shilatu huku akimuomba Katibu Mkuu Mhandisi
John Kijazi kumsaidia msanii huo ili aweze kuonana na Mhe.Rais
Dkt.Magufuli.
Januari
16 mwaka huu Msanii Rich4D alianza matembezi yake kutoka Jijini Mwanza
na kupita katika Mikoa Minane sawa na kilomita 1,200 hadi kufika Jijini
Dar Februari 10, hii ikiwa ni siku 26 mfululizo za matembezi hayo ambayo
mbali na kumpongeza Rais Dkt.Magufuli, pia yalilenga kuwasilisha kilio
cha wasanii chipukizi wa Mikoani ambao wamekuwa wakikosa fursa
mbalimbali ikilinganishwa na wasanii wakubwa walioko Jijini Dar.
“Kila Mkoa na Wilaya nilizopita nilipokelewa na
viongozi mbalimbali wakiwemo Maafisa Utamaduni na baada ya kufika Dar
nilipokelewa na Viongozi wa Serikali akiwemo aliekuwa Katibu Mkuu
Ombeni Sefue ambae aliniahidi kuonana na Mhe.Rais kabla mwezi wa mwili haujaisha kwani nilishindwa kuonana na rais baada ya kuambiwa yuko katika majukumu mengine ya Kitaifa”.
Alitanabaisha Rich4D na kumuomba Katibu Mkuu mpya Mhandisi John Kijazi kuhakikisha ahadi aliyoiacha Sefue inatimia.

Msanii Rich4D akionyesha Vibali alivyokuwa navyo kabla ya kuanza matembezi yake.
Bonyeza HAPA Kutazama Picha za Mapokezi.
0 comments :
Post a Comment