Sehemu ya mitambo ya Kinyerezi 11 inavyoonekana
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akipata maelekezo kutoka kwa wataalamu wa mitambo hiyo.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akiendelea na ukaguzi wa mitambo ya Kinyerezi 11 jijini Dar es salaam.
Waziri wa Nishati na Madini
Profesa Sospeter Muhongo akiangalia kitu kwenye kompyuta wakati
alipotembelea na kukagua ujenzi wa mitambo ya Kinyerezi 11 jijini Dar es
salaam leo.
………………………………………………………………………………………………………………….
Na Zuena Msuya, Dar Es Salaam
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ataweka jiwe la msingi katika ujenzi
wa kituo cha kuzalisha umeme cha Kinyerezi II chenye uwezo wa kuzalisha
megawati 240 unaotokana na gesi asilia iliyogundulika nchini.
Akizungumza na waandishi wa
habari jijini Dar es salaam, Waziri wa Nishati na Madini Profesa
Sospeter Muhongo,Rais Dkt Magufuli anatarajiwa kuweka jiwe la msingi
wiki ijayo machi 16, na ujenzi wa mradi huo umeanza mwezi Machi mwaka
huu na unatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miezi 28.
Prof. Muhongo alifafanua kuwa
mwanzoni mwaka 2018 ,kituo cha Kinyerezi II kitaanza kuzalisha umeme wa
megawati 240 ambapo kati ya hizo megawati 180 zitatokana na Gesi asilia
na megawati 60 zitatokana umeme utakaozalishwa kutokana na joto
litakalotokana na kuendesha mitambo ya kituo hicho.
” Mtambo huu ni wa kisasa zaidi
kwani hakuna kitakachopotea lile joto litakalokuwa linatoka kutokana na
kuendehsa mashine litazalisha umeme , tofauti na ilivyokuwa kwa
Kinyerezi I ambapo joto hupotea bure,” alisema Profesa Muhongo.
Alisema kuwa kituo hicho
kitagharimu Dolla za Kimarekani milioni 344 hadi kukamilika kwake na
tayari Mkandarasi atakayejenga kituo hicho amekwisha lipwa fedha zake
ambazo ni fedha kutoka Serikali ya Tanzania na mkopo wa bei nafuu kutoa
Serikali ya Japan.
Pia Profesa Muhongo alitumia
ziara hiyo kuuleza umma kuwa kwa sasa Serikali inaondokana na miktaba
ya malipo ya ziada ya mtaji kwa kampuni zinazoiuzia umeme (TANESCO) (
Capercity charge) kwa mikataba mipaya .
Sambamba na hilo alisema kuwa
kinachofanyika sasa ni kupitia upya mikataba iliyopo na kufanya
mazungumzo na kampuni husika ili kuondoa gharama zisizo za lazima.
Katika ziara hiyo, Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la umeme nchini (TANESCO) Mhandisi Felchesim Mramba
alisema mwishoni mwa mwezi huu kituo cha umeme cha kuzalisha umeme cha
Kinyerezi I kitaongeza uzalishaji wa umeme wa megawati 80 na hivyo
kufanya kituo hicho kuzalisha jumla ya megawati 150 kama inavyokusudiwa.
Mramba aliongeza kuwa mwanzoni
mwa mwezi April, Mkoa wa Dar es salaam , utakuwa unapata umeme moja kwa
moja kutoka Kinyerezi I tofauti na ilivyokuwa hapo awali ilikuwa
ikitegemea kupata umeme kutoka kituo cha ubungo pekee.
Mramba alisema kukamilika kwa kiasi hicho cha umeme kutapunguza kabisa tatizo la kukakatika umeme mara kwa mara nchini.
Katika ziara hiyo Profesa Muhongo
alitembelea Kituo cha umeme cha City Center pamoja na cha Mikocheni
ambavyo vitaliwezesha jiji la Dar es salaam kuondokana na nyaya za umeme
zinazopita juu.
Akimfafanua waziri Mhongo meneja
mwandamizi wa miradi ya usafirishaji na usambazaji Mhandisi Gregory
Chegere, alisema miundombinu ya umeme ya katika kituo hicho itapita
chini ya ardhi na hivyo kuondoa adha ya kukata miti pamoja na kuangushwa
kwa nguzo kutokana na mvua zitakazokuwa zinanyesha kwa jiji la Dar Es
Salaam.
Mhandisi Chegere alisema kituo
hicho kitaanza kazi mwezi April na kuuwezesha Mkoa wa Dar es salaam kuwa
na umeme wa uhakika na usiokatika.


0 comments :
Post a Comment