Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu  Hassan anatarajiwa kuwa mgeni siku ya kesho, katika kuadhimisha kilele cha Siku ya Wanawake Duniani kwa mwaka 2016, shughuli ambayo itaambagtana na semina maalum kwa wanawake wote.
Wakizungumza na wanahabari mapema leo jijini Dar es Salaam, wandaaji wa tukio hilo, kutoka Kazi Services kwa kushirikiana na Chama cha Waajili Tanzania (ATE)  pamoja na wadau wengine,
Mkurugenzi wa Kazi Services, Bi.Zuhura Sinare Muro amebainisha kuwa, Wanawake zaidi ya  400, wanatarajia kushiriki kwenye tukio hilo ambalo pia kutakuwa na semina maalum ambayo itaendeshwa na wanawake mbalimbali ambao wameweza kuthubutu n ahata kufikia malengo katika nafasia ya mwanamke.
“Tukio la kesho ya siku ya mwanamke, Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu anatarajiwa kuwa mgeni rasmi. Ambapo pia wanawake hao zaidi ya 400 watashiriki katika tukio hilo litakaloenda sambamba na semina ambayo itatolewa na wanawake wenyewe ikiongozwa na Muongeaji Mkuu, Balozi Asha Rose Migiro aliyewahi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa UN” amebainisha Bi. Zuhura Muro.
Bi. Zuhura Muro ameongeza kuwa, Maadhimisho ya  mwaka huu yanabeba Utaifa kutokana na kada hiyo ya mwanamke kupata nafasi ya kipekee kwa Mwanamke kuwa kiongozi wa juu tokea zaidi ya miaka 54 ya Uhuru wa Tanzania.
Aidha, amebainisha kuwa, baada ya kilele hicho, wanatarajia kuwa na mtandao mzuri wa wanawake kwa nchi nzima ili kuboresha vipaji vyao na waweze kuwa viongozi, watendaji na wanamama wazuri mahala pa kazi na ngazi za familia.
Tukio hilo linatarajia kufanyika kuanzia majira ya saa tisa alasiri, katika hoteli hiyo ya Serena jijini Dar es Salaam.
Imewekwa na Andrew Chale,Modewjiblog
WOMENMkurugenzi wa Kazi Services, Bi.Zuhura Sinare Muro (katikati) akizungumza wanahabari (Hawapo pichani)  mapema leo 7 Machi, akiongelea juu ya tukio hilo la siku ya Mwanamke Duniani litakalofanyika kesho katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Wengine kulia kwake ni Bi. Lilian Machela kutoka Chama cha Waajili Tanzania (ATE) na kushoto kwake ni Suzan Omari,Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano wa NHC.
WOMEN DAYMkurugenzi wa Kazi Services, Bi.Zuhura Sinare Muro (katikati) akizungumza wanahabari (Hawapo pichani)  mapema leo 7 Machi.2016, akiongelea juu ya tukio hilo la siku ya Mwanamke Duniani litakalofanyika kesho katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Wengine kulia kwake ni Bi. Lilian Machela kutoka  (ATE)  akifuatia na William Kalaghe ambaye ni mdhamini kutoka benki ya NBC. Wengine kushoto ni Bi. Jackie Namatovu mdhamini kutoka Serena Hotel) akifuatiwa na Susan Omari, mdhamini kutoka NHC.na kushoto kwake ni Suzan Omari,Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano wa NHC