Licha ya kuibuka na ushindi wa goli moja kwa bila dhidi ya timu mpya ya Rafa Benitez, Newscastle United, Leicester City imevunja rekodi aliyokuwanayo kocha Benitez tangu Agosti, 2001.
Benitez alikuwa na rekodi ya kutokupoteza mchezo wa kwanza katika timu alizofundisha ambazo ni Valencia, Liverpool, Inter Milan, Chelsea, Napoli na Real Madrid.
Goli lililomaliza historia hiyo ya miaka 15 lilifungwa na Shinji Okazaki, goli limeloisaidia Leicester kufikisha alama 63 ikiwa katika nafasi ya kwanza.