Chama cha Madereva Tanzania (TADWU) kimeelezea hisia zake kwa niaba ya madereva wa Dar es Salaam kusikitishwa na baadhi watu ambao wamekuwa wakipotosha kuwa madereva na makondakta watakuwa wakiwadhalilisha madereva kwa sababu wanapanda bure.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Madereva Tanzania (TADWU), Shaban Mdemu alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari na kueleza kuwa madereva wamepokea taarifa hizo kwa masikitiko kuwa watawanyanyasa walimu.
Ameeleza kuwa wao kama madereva wanatambua umuhimu wa elimu na pia wanatambua umuhimu wa walimu na hivyo hawawezi kuwafanyia unyanyasaji wa aina yoyote pindi watakapokuwa wakitaka kutumia daladala kwa mkoa wa Dar es Salaam.
“Kwa upande wetu madereva na makondakta, tukiwa kama wadau wakuu katika utekelezaji wa programu hii, tumeshtushwa na mtazamo ulijengeka kwa jamii dhidi yetu, baadhi yao wanatuchora kama watu ambao ni wanyanyasaji, wazalilishaji na watu ambao hatuthamini sekta ya elimu na umuhimu wa walimu kwa jamii na taifa letu. Kauli hizi zimetukera, zimetuhudhunisha na kutudhalilisha,” amesema Mdemu.
A.Mwenyekiti wa Chama Cha Madereva Tanzania (TADWU),Shaban Mdemu akizungumza na wanahabari (hawapo pichani).
Aidha mwenyekiti huyo amesema wao kama watekelezaji wa programu hiyo ya kuwapandisha walimu bure muda wa kazi wapo tayari kutoa huduma na kuwatoa hofu walimu kuwa hakuna unyanyasaji utakaofanyika na kuwataka kutumia fulsa hiyo vizuri kwa ajili ya kutimiza wajibu wao wa kazi kama inavyohitajika.
Hatua ya kuwapandisha walimu bure daladala muda wa kwenda kazini ulianzishwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda na baadae kukubaliana na Vyama vya wamiliki wa Vyombo vya Usafiri mkoa wa Dar es Salaam (DARCOBOA) na (UWADA), na unataraji kuanza kutumika Jumatatu ya Machi,7.
CWaandishi wa habari waliohudhuria katka mkutano huo wakichukua habari.