MAKUMBUSHO YA TAIFA NA SWEDEN WAANDAA ONESHO LA MATUMIZI YA ARDHI NA ATHARI ZAKE

Nkupamah media:


Makumbusho
Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Prof Audax Mabula akizungumza na waandishi wa habari. (Hawapo pichani).
hewa2This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. 600w" sizes="(max-width: 702px) 100vw, 702px" style="display: block; margin-left: auto; margin-right: auto;" />
Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Bw Achiles Bufure, kushoto kwake ni Mratibu wa Onesho la Matumizi ya Ardhi na Athari zake Bi Adelaide Salema pamoja na wanahabari mbalimbali wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho, hayupo pichani.
unnamedThis email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. 600w" sizes="(max-width: 702px) 100vw, 702px" style="display: block; margin-left: auto; margin-right: auto;" />
 Mtafiti mzamivu katika taaluma ya mazingira na matumizi bora ya ardhi kutoka Sweden Bi. Emma Li Johansson akizungumza na waandishi wa habari. hawapo pichani katika mkutano huo.
Makumbusho ya Taifa Tanzania kwa ushirikano na Chuo Kikuu cha Lund Sweden wameandaa onesho la pamoja kuhusu mabadiliko ya matumizi ya ardhi katika bonde la Kilombero. Kwa mara ya kwanza utafiti unatumia njia ya sanaa shirikishi katika kubainisha madhara ya umilikishaji wa ardhi kwa wawekezaji wakubwa dhidi ya jamii ya Tanzania.
Akizungumza na waandishi wa Habari kwenye ukumbi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa Prof Audax Mabula alitaja sababu ya onesho hili la Umoja ni kutoa elimu kwa umma juu ya mabadiliko ya matumizi ya ardhi ambayo kwa upande mwingine husababisha migogoro ndani ya jamii.
’’Afrika ni moja ya maeneo ambayo yanahodhisha ardhi kwa gharama ndogo na kutoa malipo madogo kwa wafanyakazi. Hata hivyo watafiti wengi wamekuwa wanalalamikia hali hii ya umilikishaji holela ambayo inachangia kwa kiasi kikubwa migogoro kwenye vyanzo asili na kuleta ushindani na changamoto katika jamii za maeneo athirika’’ Alisema Prof Mabula.
Prof Mabula aliongeza kuwa Watu wanayabadilisha mazingira hali ambayo huathiri watu na maisha yao. Mabadiliko ya tabia nchi, kupungua kwa maji na ubora wake, kupungua kwa mazalio ya samaki na wanyamapori, ongezeko la mifugo, vita baina ya wafugaji na wakulima ni baadhi tu ya matatizo yanayosababishwa na binadamu.
Nae Bi. Emma Li Johansson ambae ni mtafiti mzamivu katika taaluma ya mazingira na matumizi bora ya ardhi amesema onesho hili ni matokeo ya utafiti alioufanya huko Kilombero Mkoani Mprogoro kwa kutumia sanaa za maonesho kuruhusu watu kuelezea mtazamo wao juu ya matumizi na mgawanyo wa ardhi katika maeneo ya vijijini mwao.
”Lengo ni kujua namna vijiji vilivyobadilika tangu kukaribishwa kwa makampuni makubwa ya kilimo ya kigeni ambayo yamehodhi ardhi kubwa kwa ajili ya kilimo cha kisasa. Sanaa hii imetengenezwa kwa ushirikiano wa vijiji viwili athirika ambavyo vimeonesha muonekano wake wakati uliopita, sasa na mpango maendeleo kwa wakati ujao.” Alieleza Bi Emma
Akielezea program ya onesho, Mratibu wa Onesho hilo Bi Adelaide Salema amesema kuwa, pamoja na onesho hilo ,kutakuwa na mjadala kwa la lengo la kupaza sauti za wakulima wadogowadogo na kukusanya hadhara ya wadau wa kada mbali mbali katika muktadha huu kuzungumzia mabadiliko ya matumizi ardhi ili kuunda daraja baina yao na kuleta ufumbuzi wa kadhia hii.
Onesho hilo litafunguliwa rasmi tarehe 4 Machi 2016 saa tano kamili asubuhi na Bw. Jörgen Eriksson kutoka ubalozi wa Sweden nchini Tanzania katika Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni iliyopo Mtaa wa Shaaban Robert Kitalu Na. 6 mkabala na Chuo Cha Usimamizi wa Fedha (IFM) na litadumu kwa muda wa mwezi mmoja tu.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment