Steve
McClaren amefukuzwa kazi kama Meneja wa Newcastle Unite.McClaren, mwenye
Miaka 54, ametolewa kwenye wadhifa huo baada ya Miezi 9 huku Newcastle
ikiwa Nafasi ya 19 kwenye Ligi Kuu England ikiwa ni nafasi 1 tu juu ya
Timu ya mkiani Aston Villa.
Tangu McClaren atwae wadhifa huo mwanzoni mwa Msimu huu Newcastle imeshinda 7 tu kati ya 30.
Mechi ya
mwisho kwa McClaren ilikuwa Jumamosi iliyopita Newcastle wakiwa kwao St
James Park na kupigwa 3-1 na Bournemouth ikiwa ni kipigo chao cha 5
katika Mechi 6 zilizopita.
Habari za ndani ya Newcastle zinamtaja Rafael Benitez, Meneja wa zamani wa Chelsea, Liverpool na Real Madrid, kumrithi McClaren.
Inaaminika
Muhispania huyo huenda akateuliwa haraka na kutwaa wadhifa kabla
Newcastle haijasafiri kwenda huko King Power Stadium Jumatatu Usiku
kucheza na Leicester City.(VICTOR)
ENGLAND – Ratiba Mechi za Wikiendi
**Saa za Bongo
Ijumaa Machi 11
EMIRATES FA CUP – Raundi ya 6 [Robo Fainali]
2255 Reading v Crystal Palace
Jumamosi Machi 12
LIGI KUU ENGLAND
1545 Norwich v Man City
1800 Bournemouth v Swansea
1800 Stoke v Southampton
EMIRATES FA CUP - Raundi ya 6 [Robo Fainali]
2030 Everton v Chelsea
Jumapili Machi 13
LIGI KUU ENGLAND
1900 Aston Villa v Tottenham
EMIRATES FA CUP - Raundi ya 6 [Robo Fainali]
1630 Arsenal v Watford
1900 Man United v West Ham
Jumatatu Machi 14
LIGI KUU ENGLAND
2300 Leicester City v Newcastle


0 comments :
Post a Comment