Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni DC PAUL MAKONDA Atoa Siku 14 Barabara za Kinondoni Zizibwe Mashimo la Sivyo Watakiona Cha Moto


MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda jana alifanya ziara ya kukagua barabara ya Mwanayama 'A' hadi Makumbusho ambayo imeharibika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
Akizungumza baada ya kukagua barabara hizo alisema amewapa watendaji wa manispaa ya Kinondoni wiki mbili kushughulikia tatizo hilo kutokana na adha ya magari yanayotumia barabara hiyo.

"Sasa nimeiagiza Manispaa, nimewapa wiki mbili kuhakikisha mashimo yote yawe yamezibwa, na wakishindwa nitawasaidia kuwawajibisha na kuchukua hatua stahiki." Alisema Paul Makonda

Alisema kuwa kuharibika kwa barabara nyingi katika manispaa hiyo ni kutokana na kujengwa chini ya kiwango.

Makonda alisema fedha zinatolewa kwa ajili ya ujenzi lakini baadhi ya watendaji wanajenga chini ya kiwango na kuwapa adhabu wananchi wanaotumia barabara hiyo
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment