Aprili 2.2016  kunatarajia kufanyika tukio la aina yake la msimu was aba wa Pop Up Bongo ambapo kutakuwa na mauzo kwa watu mbalimbali kujumuika kufanya manunuzi na kuuza bidhaa tofauti tofauti zikiwemo zile za nyumbani sambamba na tukio la muziki kutoka kwa Dj maarufu Bongo.
Pop Up Bongo ni tukio la kipekee linalofanyika nchini huku likikusanya watu mbalimbali pamoja na kupata taarifa muhimu za bidhaa pamoja na masoko huku wakiburudika na muziki mzuri kutoka kwa Dj’s na ‘tip’ nyingine za masoko ya ndani na nje ya nchi.
 tukio hilo ambalo linatarajia kufanyika Jumamosi ya wiki ijayo ya Aprili 2.2016,  ndani ya Dar- tuk tuk thai, watering hole patio watu wote wanakaribishwa na ni bure.
Pop Up Bongo tokea kuanzishwa kwake, limekuwa likipanua wigo mpana kwa washiriki wake wanauza  bidhaa zao kwani watu wa ndani na mataifa ya nje wamekuwa wakimiminika huku pia wakipaata kujitangaza Zaidi ndani na nje ya Mataifa mbalimbali. Pia waweza kutembelea mtandao wa: popupbongo.com
12291027_1735089216712840_1134421639925227523_oMoja ya matukio ya Pop Up Bongo katika misimu iliyopita. 
12304469_1735085453379883_7444987953583420217_oPop Up Bongo moja ya matukio ya misimu iliyopita wafanyabiashara wakinunua na kuuza
Msimu wa saba wa POP UP BONGO umewadia, kufanyika  Aprili 2, Dar- tuk tuk thai,12322467_1735084110046684_5385293735474408854_oPop Up Bongo moja ya matukio ya misimu iliyopita wafanyabiashara wakinunua na kuuza. (Picha zote kwa hisani ya mtandao wa Pop Up Bongo).